je! umeitii agizo kuu ilio amri
ya
mungu?
mathayo 28: 18-20
Kif. 18; Yesu alikuwa na uwezo wote, binguni na hata duniani; yamaanisha ya
kwamba pangekuwa na wengine wawili pamoja naye hawangekua na uwezo
wowote.
Kif. 19; Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa
jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.
Kif. 20; "na kuwafundisha kuyashika yote niliowaamuru ninyi". Tafadhali tazama
matamshi haya ----- Yesu hakusema wabatizwe kwa maneno, "Baba, Mwana
na Roho Mtakatifu".
Tunajuwa ya kwamba jina la mwana ni "Yesu" na ya kwamba alikuja kwa jina la babake (Yohana 5:43)
Ikiwa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu sio viuembe vitatu, je wao ni akina
nani?
Isaia 9:6 ----- Nabii Isaia hujibu swali hili kinaganaga; huyu Mwana (Yesu) ataitwa
" Mshauri wa Ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba na Milele Mfalme wa Amani.
Mshauri ----- Mfariji
Yohana Mtakatifu 14:26
Katika Biblia ya aina ya "New International Version" na ya "Amplified Version"
na zinginezo, neno "Mshauri" limetumika badala ya "Mfariji".
Inajulikana kwa kila mtu ya kwamba mfariji ni huyo Roho Mtakatifu yaani Roho wa Kristo aliepaa binguni. Yohana 14:16-18.
Mungu aliye na uwezo
Isaia alimwita kwa jina "Mungu alie na uwezo".
Ufunuo 1:8
Yesu anajiita mwenyewe "Mungu alie na uwezo wote."
Ufunuo 4:8 na 11:17, walimsujudu yeye na kumwita Baba "Mungu Mweza Yote."
Baba Alie Wamilele
Wakati Yesu alikua duniani alikua mwenye asili mbili; alikua mwanadamu na pia
Mungu; Roho wake ndiye alikua muumba wa vitu vyote (Yohana 1:3,
Wakorosai 1:16,17).
Isaia 44:24 Ya eleza ya kwamba Mungu ndiye aliviumba vitu vyote, yeye mwenyewe akiwa
pekee.
Maandiko haya ya Biblia yadhibitisha ya kwamba Yesu alie Mungu katika agano
jipya ndiye yule aliyekua Mungu katika agano la kale.
Kwa hivyo jina, "Bwana Yesu" ni lazima liwe ndilo jina la Baba, na la Mwana
na tena la Roho Mtakatifu.
siri ilio kuu
1 Tim. 3:16 Paulo atuzungumizia juu ya Siri ilio kuu ya Uungu; ya kwamba Mungu alifanyika mtu na akakaa kati ya wanaadamu.
Soma Yohana 1:14 ni kama fumbo lililo kubwa;
Ni lazima tulinganishe vifungu vyote vya Biblia pamoja ilitupate mfano dhahiri na
hasili ya Mungu.
Yohana 14:25,26
Kif. 25 ----"Hiyo nimesema nanyi kwa mithali; saa yaja ambayo sitasema nanyi tena
kwa mithali; lakini nitawapa waziwazi habari ya Baba.
Kif. 26 ----" Na siku ile mtaomba kwa jina langu; wala siwaambii ya kwamba mimi
nitawaombea kwa Baba," wakati huu akiwa ametukuzwa na Babake, na hali yake
ya kua "Mungu ndani ya mwili wake" itakua imefika kikomo.
Maandiko yake mariko
Mariko 16:15-17
Yesu aliaamuru mitume wake.
Kif.15 ---Enedeni ulimwengu mwote mkaihubili injili kwa kila kiumbe."
Kif.16 ---"Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiye amini, atahukumiwa."
Kif.17 ---"Kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya,"
Viongozi wengi hodari wakidini hufundisha ya kwamba mtu anaeokolewa kwa
kumwamini Bwana Yesu na kumkubali kama mwokozi; fundisho hili linaweza kuaje
haliandamani na "agizo kuu pamoja na "Amri zake Mungu ---
Kulingana na Maandiko ya Luka
Luka 24:45
----Yesu ndipo aliwafunua akili zao iliwapate kuelewa maandiko.
Kif.47 ---"Mataifa yote watahubiriwa Kwa Jina lake habari ya toba na ondoleo la
dhambi, kuanza tangu Yerusalemu."
Kif.49 ---"nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni njini hata mvikwe
uwezo utokao juu."
Matendo 1:8 Walipokea uwezo huu walipobatizwa kwa Roho Mtakatifu.
Walimtii Yesu
Matendo 1:4 Waliamurishwa wakae Yerusalem mpaka wampokee Roho Mtakatifu.
Matendo 1:13-15 Mitume wote pamoja na wanafunzi na hata Mariamu mamake Yesu,
waliitii amri.
Kif.25 ---kwa jumla walikuwa wamekusanyika waaminio mia moja na ishirilini.
Yalio Tokea---
Matendo 2:1-4
"Siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja."
Kif.4 ---"Wote wakajazwa Roho Mtakatifu wa kaanza kusema kwa lugha
nyingine, kama Roho alivyo wajalia kutamka."
Kulikuwa na umati mkubwa Yerusalemu wakati huo kila mmoja wao alishangaa kuona na kusikia yaliotokea.
ilio agizo
Matendo 2:14-36----Petro akiwa ndiye nwenye funguo za ufalme, alihubili ujumbe wa kusandikisha
sana kwa ule umati ulio kusanyika.
Kif.37 ---walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na
mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
Kif.38 ---wakati huo "Petro akawaambia, tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu."
Kif.39 ---"A hadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote
walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie." Rafiki,
hata ikiwa ni miaka zaidi ya elfu mbili imepita ujumbe huu una tuhusu.
Kif.41 ---Wale wote walio upokea ujumbe wake Petro walimbatizwa siku hiyo;
na kundi la waaminio likaongezeka na watu elfu tatu.
Mlango Uwazi Kwa Mataifa
Matendo 10:1-48---Kwa maono, mchaji Mungu aliyeitwa Kornelio alitembelewa na malaika
ambaye alimwambia amtume mtu akamuita Petro. Alimwambia ya kwamba
Petro ndiye atakae mueleza yampasayo kutenda.
Fahamu tafadhali Matendo 11:14
---"atakayekwambia maneno ambayo yatakuokoa wewe na nyumba yako yote."
Kwa wakati ule ule Petro alipata maono kutoka kwa Bwana akionyeshwa ya
kwamba wokovu huu mkuu ulikuwa wa mataifa pia.
Petro alienda nyumbani kwa Kornelio na kumhubiria juu ya Yesu, kifungu cha 44-
46 -- "Petro alipokuwa akisema maneno haya Roho Mtakatifu akawashukia
wote waliolisikia lile neno, --- kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha na
kumwadhimisha Mungu."
Ubatizo Ukatika Amri
Vifungu 47-48 ---"Ni nani awezaye kukataza maji, hawa wasibatizwe, watu aliopokea Roho
Mtakatifu vile vile kama sisi? Akaamuru wabatizwe, kwa Jina lake Yesu Kristo.
swali
Je huoni amri hii ina kuelekea pia, hata ikiwa umepokea Roho Mtakatifu na huja batizwa
kwa jina la Yesu?
Kumbuka hakuna jina lingine nduniani limepeanwa liwezalo kutuokoa! (Matendo 4:12).
Kuzaliwa Mara Ya Pili
Yohana 3:3-7 ---Yesu alimwabia Nikodemo yakwamba hangeweza kuona wala kuingia katika ufalme wa Mungu iwapo haja zaliwa mara ya pili.
Nikodemo akamwuliza Bwana, "Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee?"
Kif.5 ---Yesu akasema, Amini amini nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kwingia ufalme wa Mungu.
Kif.7 ---Yesu mwenyewe aliitamka amri, "Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.
Rafiki ukweli wa neno la Mungu umekwishawekwa mbele yako; sasa ukweli u mikononi mwako; usiupinge.
kijitabu cha: lewis e. manuwal
kiituacho: "have you obeyed the great commission. which was a command of god
kutafsiriwa na
huduma ya: Vision for the Lost Souls Centre Ministries Inter.
P.O. Box 283 - 00300 RN
nairobi
Tel: 0722-357710, 0722-837558, 0721-495200
Email: vlsministries1999@yahoo.com
© 2003